Ifahamu mikoa 10 inayoongoza kwa uzazi wa mpango Tanzania

Dar es Salaam. Miongoni mwa masuala yanayogusa zaidi vijana wengi waliopo kwenye ndoa na wasio kwenye ndoa kwa sasa ni suala la kuwa na watoto. 

Miongoni mwa maswali makubwa huwa ni lini wapate watoto, idadi ya watoto lakini ni njia gani sahihi itakayomfanya wanawake vijana wasipate ujauzito bila kutarajia. Wataalamu wanasisitiza kuwa ni vema wazazi vijana wakapanga mipango yao vema ya kijamii na kiuchumi kabla ya kupata watoto. 

Hata hivyo, si watu wote wanapanga ipasavyo juu ya kupata watoto. Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria wa mwaka 2022 unabainisha kuwa nchini Tanzania takriban wanawake wanne kati ya 10 au asilimia 38 ya waliolewa wenye umri wa miaka 15 hadi 49 wanatumia njia ya aina yeyote ya uzazi wa mpango.

Ripoti ya utafiti huo uliofanywa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kwa ushirikiano na taasisi nyingine iwepo Wizara ya Afya inabainisha ipo baadhi ya mikoa yenye kiwango kikubwa cha wanawake wenye wanaotumia ipasavyo njia za uzazi wa mpango ikiongozwa na Njombe huku mingine ikitumia kwa kiwango kidogo sana kama Simiyu. 

Je, waifahamu mikoa inayoongoza kwa matumizi ya njia za uzazi wa mpango Tanzania? 

Ahueni: Bei ya petroli, dizeli, mafuta ya taa zikishuka

 

  • Bei ya rejareja ya petroli imeshuka kwa Sh187 kwa lita.
  • Wakazi wa Dar es Salaam sasa watanunua lita moja kwa Sh2,781 kutoka Sh2,968 ya Machi.

Dar es Salaam.Watumiaji wa vyombo vya moto sasa watakuwa na ahueni baada ya bei za mafuta mwezi Aprili kushuka kwa kiwango kikubwa ikilinganishwa na ilivyokuwa mwezi uliopita.

Bei mpya kikomo zilizotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura) zinabainisha kuwa bei ya rejareja ya petroli liyoingizwa kupitia Bandari ya Dar es Salaam imeshuka kwa Sh187, kwa lita huku ile ya dizeli ikipungua kwa Sh284 kwa lita na mafuta ya taa yakipungua kwa Sh169 kwa lita.

Wamandavaku

Maandazi sio mchuzi

Ms Mbesse akamatwa

Bei ya mazao ya paa