Ahueni: Bei ya petroli, dizeli, mafuta ya taa zikishuka

 

  • Bei ya rejareja ya petroli imeshuka kwa Sh187 kwa lita.
  • Wakazi wa Dar es Salaam sasa watanunua lita moja kwa Sh2,781 kutoka Sh2,968 ya Machi.

Dar es Salaam.Watumiaji wa vyombo vya moto sasa watakuwa na ahueni baada ya bei za mafuta mwezi Aprili kushuka kwa kiwango kikubwa ikilinganishwa na ilivyokuwa mwezi uliopita.

Bei mpya kikomo zilizotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura) zinabainisha kuwa bei ya rejareja ya petroli liyoingizwa kupitia Bandari ya Dar es Salaam imeshuka kwa Sh187, kwa lita huku ile ya dizeli ikipungua kwa Sh284 kwa lita na mafuta ya taa yakipungua kwa Sh169 kwa lita.

Unatumia saa ngapi kufanya kazi kwa wiki?

.

  • Wafanyakazi wanaolipwa na waliojiajiri wenyewe (wenye wafanyakazi na wasio na wafanyakazi) wanatumia muda mwingi kazini ikilinganishwa na makundi mengine.

Dar es Salaam. Licha ya muda wa kufanya kazi kwa watu waliopo kwenye ajira kupungua Tanzania, wafanyakazi wanaolipwa na waliojiajiri wanafanya kazi muda mwingi kuliko makundi mengine.

Kwa mujibu wa ripoti ya Utafiti wa Uwezo wa Kufanya Kazi Tanzania (ILFS) ya mwaka 2020/21 iliyotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (OCGS), muda wa kawaida wa kazi umepungua kidogo kutoka wastani wa saa 54 kwa wiki mwaka 2014 hadi saa 53 mwaka 2020/21.

Kupungua kwa muda wa kawaida wa kazi kati ya mwaka 2014 na 2020/21 kumeonekana zaidi kwa wanawake kuliko wanaume. Hali hii inachangiwa na wanawake kutumia muda mwingi katika shughuli za kijamii. 

Hata hivyo, masaa ya kufanya kazi yanaendana na viwango vya kimataifa vinavyotolewa na Shirika la Kazi Duniani (ILO) vya kufanya kazi kati ya saa 48 na 56 kwa wiki.

Aidha, matokeo ya utafiti huo yanaonesha kuwa wafanyakazi wanaolipwa na waliojiajiri wenyewe (wenye wafanyakazi na wasio na wafanyakazi) wanatumia muda mwingi kazini ikilinganishwa na makundi mengine

Saa za kazi ni kipimo cha wastani wa muda ambao watu hutumia kwenye shughuli za uzalishaji wa bidhaa na huduma. Uchambuzi wa muda wa kazi umefanyika kwa kuangalia Saa za Kazi za Kawaida (Usual Hours of Work) na Saa za Kazi za Sasa (Current Hours of Work).

Ms Mbesse akamatwa

Bei ya mazao ya paa