Filamu nyingine ya kufunga mwaka 2019 yaingia sokoni

December 16, 2019 7:31 am · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link

Hata baada ya kuwasili kwenye pori la Jumanji, hali inazidi kuwa ngumu zaidi kwani yule aliyetakiwa kuwa Spencer kwenye mchezo huo siyo Spencer tena. Picha| Freekingeek.


  • Filamu hiyo ya Jumanji: Welcome To The Jungle inawahusisha watani Kelvin Hart na Dwayne Johnson.
  • Imeingia kwenye kumbi za sinema tangu Disemba13.
  • Inafundisha umuhimu wa marafiki kwenye maisha.

Dar es Salaam. Baada ya Spencer (Alex Wolf) na marafiki zake Bethany (Madeson Iseman), Martha (Morgan Tumer) na Anthony (Ser’Darius Blain) kuwa marafiki baada ya kushiriki safari ambayo hawakuitarajia kwenye Jumanji: Welcome To The Jungle, safari nyingine inawaita.

Hata hivyo, mambo yanazidi kubadilika kwenye “Jumanji: Next level” ambapo Martha, Bethany na Anthony wanatakiwa kurudi tena ndani ya mchezo wa Jumanji kumuokoa rafiki yao Spencer ambaye anaonekana kucheza mchezo huo bila kuwashirikisha.

Hata baada ya kuwasili kwenye pori la Jumanji, hali inazidi kuwa ngumu zaidi kwani yule aliyetakiwa kuwa Spencer kwenye mchezo huo siyo Spencer tena. Na hata Anthony, ambaye alitakiwa kuwa ndani ya mwili wa Kelvin Hart, anajikuta kwenye mwili uliokuwa wa Betany.

Ndiyo, inachanganya kihivyo lakini unaweza kujibu maswali yako kwa kununua tiketi yako kwenye kumbi za sinema zinazopatikana kwenye kumbi za kuangalizia filamu zikiwemo za Mlimani City, Aura Mall na Mkuki House.

Unaachaje kuona kisa hiki kinachomhusisha Dwayne Johnson alieshiriki kama Dk Smolder na Kelvin Hart aliyeshiriki kama Franklin Finbar? Zaidi, kikiongozwa na Jake Kasdan ambaye anakadiriwa kutumia bajeti ya Sh346.2 bilioni ili kuboresha msimu wako wa sikukuu?

Tembelea kumbi tajwa kuiona filamu hii ambayo ipo kwenye skrini za kumbi za sinema za Century Cinemax tangu Disemba13, 2019.


Zinazohusiana


Filamu ya Jumanji ni kati ya filamu nne ambazo zilikuwa zinasubiriwa kwa hamu kutoka mwishoni mwa mwaka huu.

Hadi sasa, kati ya filamu hizo, Jumanji inaweka alama ya filamu ya tatu katika orodha ya filamu hizo baada ya filamu za Gemini Man na Frozen II kutikisa kumbi za filamu kwa siku zilizopita. 

Huenda, filamu ya Star Wars, The rise of Skywalker ambayo iko njiani kutoka ikafunga mwaka katika orodha ya filamu hizo nne. Filamu hii iko chini ya Jeffrey Abrams ambaye ni kiongozi wa filamu ya “Mission Impossible” na “Overload” za mwaka 2018.

Star Wars ni mfululizo wa filamu tatu ambazo zinaelezea hadithi isiyo halisi. Kutana na Daisy Ridley, Carrie Fisher, Mark Hamill na John Boyega kujua kama kuna mwisho wa mapambano Rey, Fin na Poe walio na nguvu na maarifa kutoka vizazi vya zamani.